IQNA

Maonyesho ya Shamim Hussein Yazinduliwa Tehran

TEHRAN (IQNA)- Maonyesho maalumu yamezinduliwa katika eneo la Rey, kusini mwa Tehran kwa lengo la kuonyesha vifaa vinavyotumika katika maombolezo ya Muharram.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wakfu ya Tehran na maafisa kadhaa wa serikali walishiriki katika uzinduzi huo katika jengo la kaburi la  Sheikh Saduq huko Rey.

Muharram ni mwezi wa kwanza wa kalenda ya Hijria Qamaria.

Kila mwaka katika mwezi wa Muharram, Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia, hukumuka kuua shahidi Imamu wa Tatu wa Mashia, ambaye ni mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS ambaye aliuawa shahidi katika vita vya Karbala, kusini mwa Iraq akiwa pamoja na wafuasi wake watiifu 72. Imam Hussein AS aliuawa shahidi akiwa anapigana kupinga dhulma ya utawala wa Yazid ibn Muawiya.

 
 
Kishikizo: imam hussein as ، muharram ، karbala