IQNA

Rais wa Tunisia apinga uingiliaji wa kigeni katika mgogoro nchini humo

21:10 - September 11, 2021
Habari ID: 3474283
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Tunisia Kais Saied amesema nchi yake haitastahamili uingiliaji wowote wa kigeni huku akiwa chuni ya mashinikizo kutoka kwa madola ya magharibi kufungua tena bunge la nchi hiyo.

Amesisitiza kuwa mamlaka ya dola la Tunisia na chaguo la watu wake ni mambo ambayo hayawezi kujadiliwa na washirika wa kimataifa.

Tunisia ilitumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa mwezi uliopita baada ya Rais Kais Saied wa nchi hiyo kumfuta kazi Waziri Mkuu, kusimamisha shughuli za Bunge la kutwaa madaraka yote ya nchi.

Kais Saied alisema sababu ya maamuzi hayo ni utendaji mbaya wa serikali katika suala la kupambana na maambukizi ya corona na hali mbaya ya kiuchumi. 

Hata hivyo vyama vya siasa na wananchi wengi wa Tunisia wanasema kuwa, hatua hiyo ya Rais Kais Saied imekiuka Katiba na sheria za nchi. Taasisi 7 za kiraia za Tunisia zimepinga vikali maamuzi ya kiongozi huyo zikisema amefasiri isivyo kifungo nambari 80 cha Katiba.

Madola ya Umoja wa Ulaya na Marekani yamekuwa yakimshinikiza Rais Saied kusitisha hatua zake. Hatahivyo Rais Saied amesema hatua alizochukua ni kwa mujibu wa katiba na hivyo amesisitiza kushikilia msimamo wake.

Kishikizo: tunisia saied
captcha