IQNA

Tilawa ya hivi karibuni ya Ustadh Abulqasimi ya Surat Al-Fath + Video

TEHRAN (IQNA)- Hivi karibuni klipu ya Ustadh Ahmad Abulqasimi, mwalimu na qarii wa kimataifa Muirani akisoma Surat Al Fath imesambazwa.

Ifuatayo hapa ni klipu ya Ustadh Abulqasimi akisoma  aya za 7 hadi 10 ya Surat Al Fath na halikadhalika aya za 5 hadi 9 ya Sura Insan na pia qiraa ya Sura Al Kauthar.

 

 

وَلِلَّهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

Na Mwenyezi Mungu ana majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا

Hakika tumekutuma wewe uwe Shahidi, na Mbashiri, na Mwonyaji,

 لِتُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُ وَتُسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا

Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumhishimu, na mumtakase asubuhi na jioni.

 إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّهَ يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَنْ نَكَثَ فَإِنَّمَا يَنْكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا

Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Basi avunjaye ahadi hizi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake; na anaye tekeleza aliyo muahadi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa. (Surat Al Fath 7-10)

3995595/

Kishikizo: qiraa ، abulqasemi ، iran