IQNA

Msikiti wahujumiwa eneo la Manchester nchini Uingereza

14:08 - September 12, 2021
Habari ID: 3474286
TEHRAN (IQNA) - Polisi wanachunguza shambulio la kuchoma moto msikiti huko Greater Manchester, Uingereza.

Hujuma dhidi ya msikiti huo imetajwa kuwa ni uhalifu wa chuki.

Maafisa wa usalama walifika eneo la tukio baada ya ripoti moto katika msikiti wa Didsbury, ulio kwenye makutano ya Barabara ya Barlow Moor na Barabara y a Burton Road,  usiku wa manane Jumamosi.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika moto huo, ambao ulisababisha uharibifu mdogo kwa mlango wa msikiti. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji la Greater Manchester limesema walikuwa katika eneo la tukio kwa zaidi ya masaa mawili, wakifanya uchunguzi wa pamoja na polisi.

Watu wawili wapitanjia walijaribu kuzima moto kwa makoti yao, kulingana na chapisho kwenye ukurasa wa Facebook wa msikiti, ambao uliongeza: "Tunawashukuru sana na kutoka moyoni mwetu, 'Asante'."

Afisa msimamizi wa msikiti huo, Tracey Pook, aliiambia Manchester Evening News kwamba "hawezi kuwashukuru vya kutosha". Aliambia gazeti hilo kuwa: "Chuki haina nafasi katika jamii yetu ... Hatutaruhusu chuki ishinde - tutaendelea kama kawaida, tutaendelea kufanya miradi yetu na kufanya mema kwa jamii yetu. Huo ni Uislamu - kuwa mwema na kuonyesha wema. "

Inspekta  Shoheb Chowdhury kutoka polisi wa Greater Manchester alisema: "Hili ni tukio la kutisha ambalo bila shaka litasababisha wasiwasi katika jamii na tunafanya kila tuwezalo kupata ni nani aliyehusika sambamba na kuendelea kushirikiana msikiti na wale wanaohusika katika jamii.

"Wapelelezi wamekuwa wakifanya uchunguzi na  tayari wamechukua taarifa za kamera za siri za CCTV katika eneo la tukio kama sehemu ya uchunguzi.”

“Uhalifu wa chuki hautavumiliwa. Tuna bahati kwa kuwa Greater Manchester ni sehemu ya watuy kutoka jamii  na huita eneo hili nyumbani na wale ambao wanataka kufanya uhalifu unaosababishwa na chuki watafikishwa mahakamani.

Afzal Khan, mbunge wa Manchester Gorton, ameandika katika ukurasa wake wa  Twitter kuwa: “Nilishtuka kusikia kuhusu jaribio la kuchoma moto msikiti wa Didsbury jana usiku. Tunashikamana na dugu na dada zetu.  Mashambulizi yatokana na Islamophobia (chuki dhidi Uislamu) ambayo yanalenga misikiti yanaongezeka. " Aliwauliza watu "wakae macho" na waripoti visa kwa polisi na jumuiya ya kijamii ya Tell Mama, ambayo huwasaidia wahasiriwa wa chuki dhidi ya Waislamu nchini Uingereza.

3475687

captcha