Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Jumba la Makumbusho la Louvre Abu Dhabu kwa ushirikiano na Jumba la Kitaifa la Makumbusho Guimet la Ufaransa kwa himaya ya Jumba la Makumbusho la Ufaransa. Maoneysho hayo yataonyesha maingiliano ya kiutamaduni na kisanaa baina ya staarabu za China na ulimwengu wa Kiislamu kuanzia karne za 8 hadi 18 Miladia.
Maoneysho hayo yatawasilisha taswira za maingiliano ya staarabu hizo mbili kuanzia Bara Arabu, Asia ya Kati, Bahari ya Hindi hadi China na Vietnam ambapo yatadhihirihsa taswira ya uhusiano mrefu na tajiri.