IQNA

Mkutano wa Idhaa za Qur’ani za nchi za Kiislamu kufanyika Cairo

10:34 - September 14, 2021
Habari ID: 3474294
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Nchi za Kiislamu (ISBO) na Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar wametangaza azma ya kuandaa kikao cha Idhaa za Qur’ani za nchi za Kiislamu mwezi Februari mwaka 2022.

Kwa mujibu wa taarifa Sheikh Mkuu wa Al Azhar Sheikh Ahmad al-Tayyib ammeysema hayo mnamo Septemba 12 mjini Cairo, Misri alipokutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa ISBO Amru Allaithi.

Pande mbili zilijadili njia za kuimarisha ushirikiano katika uga wa kidini na vyombo vya habari kwa ajili ya kuwapa Waislamu fursa ya kuufahamu Uislamu kwa njia bora.

Wawili hao walisisitiza umuhimu wa kutumia uzoefu wa Al Azhar na taasisi zake tanzu katika masuala ya vyombo vya habari.

Kati ya yaliyoafikiwa katika kikao hicho ni kuitisha kikao cha wakurugenzi wa Idhaa za Qur’ani chini ya usimamizi wa Al Azhar na kwa ushirikiano wa ISBO.

Halikadhalika Al Azhar imeafiki kutayarisha jumbe za kidini ambazo zitarushwa hewani na kanali zinazofungamana na ISBO.

Shirika la Utangazaji la Nchi za Kiislamu (ISBO) lilianzishwa Jeddah Saudi Arabia mwaka 1975 ni liko chini ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu (OIC).

3997112

captcha