IQNA

Tafsiri ya kale ya Qur’ani katika Maktaba la Alexandria

13:44 - September 15, 2021
Habari ID: 3474297
TEHRAN (IQNA)- Tafsiri ya kale ya Qur’ani Tukufu inahifadhi katika Jumba la Makumbusho la Nyaraka za Kale la Alexandria nchini Misri.

Tafsiri hiyo ya lugha ya Kiarabu imeandika na Abu Ishaq bin Ibrahim ambaye pia anakulikana kama al-Busti.

Nakala hiyo hivi sasa inakarabatiwa katika maabara na inaaminika kuwa iliandikwa mwaka 368 Hijria Qamaria sawa na 978 Miladia.

Katika tafsiri hiyo mwandishi anaandika aya au sehemu yake na kisha anataja Hadithi na baada ya hapo anafasiri aya.

Tafsiri hiyo ni muhimu kwani inaonyesha pia namna maandishi ya Kiarabu yalivyobadilika.

Katika Jumba la Makumbusho la Nyaraka za Kale la Alexandria nchini Misri, kuna idadi kubwa ya nyaraka  miaka 1,000 iliyopita.

3997642

captcha