IQNA

Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu kufunguliwa Turin, Italia

22:09 - September 23, 2021
Habari ID: 3474332
TEHRAN (IQNA)- Eneo la kiviwanda la Turin, ambao ni kati ya miji mikubwa Italia, hivi karibuni litakua na fahari ya kupata kituo kikubwa cha utamaduni wa Kiislamu ambacho kitajumuisha pia msikiti.

Kwa mujibu wa taarifa, taasisi ya Wakfu wa Kiislamu Italia imenunua jengo la kituo hicho kwa Euro milioni moja. Jengo hilo ambalo liko karibu na karakana za Shirika la Magari la Fiat.

Taasisi ya Wakfu wa Kiislamu Italia imesema kituo hicho cha Kiislamu kitakuwa kinatoa mafunzo mbali mbali kwa lengo la kustawisha ufahamu wa utamaduni wa Kiislamu miongoni mwa Waislamu.

Tayari mji wa Turan una misikiti 15 na inakadiriwa kuwa kuna Waislamu 60,000 mjini humo ambapo karibu nusu yao ni kutoka Morocco.

3475765

captcha