IQNA

Msomi: Uislamu unasisitiza kulinda maeneo ya ibada hata ya wasio Waislamu

18:48 - October 25, 2021
Habari ID: 3474470
TEHRAN (IQNA)- Msomi wa Kiislamu nchini Misri amesema Uislamu unalipa umuhimu mkubwa suala la kulinda maeneo ya ibada hata yale ambayo si ya Waislamu.

Akihutubu katika warsha iliyojadili aya za Qur'ani ambazo hutumiwa vibaya na watu wenye misimao mikali ya kidini kutetea hujuma zao dhidi yaw engine, Profesa Abdul Fattah al Awari amesema ni wajibu wa Waislamu kulinda misikiti na maeneo mengine ya ibada.

Amesema  kwa mujibu wa mafundishi ya Kiislamu, ni wajibu kulina maeneo ya ibada hata yale ambayo si ya Waislamu.

Al Awari wakati mmoja walikuwa naibu mkuu wa Kitivo cha Usuluddin katika Chuo Kikuu cha Al Azhar amelaani vikali namna wale wenye misimamo mikali ya kidini wanavyofasiri vibaya aya za Qur'ani.

4007753

captcha