IQNA

Algeria yazindua 'Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani'

17:35 - October 27, 2021
Habari ID: 3474477
TEHRAN (IQNA) – 'Wiki ya 23 ya Kitaifa Qur'ani' nchini Algeria imezinduliwa katika sherehe iliyofanyika Jumanne.

Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya Nahar Online, sherehe za uzinduzi wa wiki hiyo zilihudhuriwa na Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini Yusuf Bilmahdi.

Shughuli zote za Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani nchini Algeria zinafanyika kwa usimamizi wa Rais Abdelmadjid Tebboune wa nchi.

Nara na Kauli Mbiu ya Wiki ya Qur'ani Algeria mwaka huu ni "Mapenzi kwa Nchi, Mtazamo wa Kimaadili na Kufungamana Kitaifa." Eneo la Klabu ya Kitaifa ya Jeshi mjini Algiers ndio mwenyeji wa 'Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani'.

Kati ya shughuli za wiki hiyo ni pamoja na mashindani ya kitaifa ya kuhifadhi, kusoma na kutafsiri Qur'ani Tukufu. Algeria ni nchi kubwa katika ukanda wa kaskazini mwa Afrika na karibu asilimia 99 ya watu wake ni Waislamu.

4008249

Kishikizo: algeria Bilmahdi qurani
captcha