IQNA

Watu wa Qatar kushiriki Sala ya Istisqa

18:24 - October 27, 2021
Habari ID: 3474479
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar imetangaza kuwa, Sala ya Istisqa yaani Swala ya Kuomba Mvua itaswaliwa nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa  Sala hiyo itasaliwa Alhamisi Oktoba 28, 2021 saa kumi na mbili kasorobo Alfajiri.

Sala hiyo inatazamiwa kusaliwa katika misikiti 90 kote katika nchi hiyo.

Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani  atasalisha sala hiyo katika Uwanja wa Sala wa  Al Wajba.

Qatar imekuwa ikishuhudia uhwaba mkubwa wa mvua katika miaka ya hivi karibuni.

3476227

Kishikizo: sala Istisqa qatar
captcha