IQNA

Israel yaonywa kuhusu kubomoa makaburi ya al-Yusufiya mjini Quds

18:34 - October 27, 2021
Habari ID: 3474480
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina yameuonya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuhusiana na kuendelea uvamizi na hujuma dhidi ya maeneo matakatifu ya Kiiislamu huko Palestina hususan maziara makaburi ya al-Yusufiya huko Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Makundi ya muqawama Palestina yamesema katika taarifa yao kwamba, Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wanapaswa kutumia nyenzo na suhula za aina yoyote ile kwa ajili ya kukabiliana na adui Mzayuni.

Taarifa hiyo inaripotiwa kukiwa na taarifa za vitendo vya walowezi wa Kizayuni kuvunja na kubomoa makaburi ya Waislamu ya al-Yusufiya huko Palestina.

Sehemu nyingine ya taarifa ya makundi ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina imebainisha kwamba, maadui wavamizi wanapaswa kutambua kwamba, kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina na kufanya hujuma dhidi ya maeneo matakatifu kuna gharama zake tena kubwa.

Aidha makundi ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina yamezitaka asasi za jumuiiya za kimataifa kuchukua hatua za haraka na za maana kwa ajili ya kuwaokoa mateka wa Kipalestina sambamba na kukomesha hujuma za Wazayuni dhidi ya maeneo matakatifu huko Palestina.

Hivi karibuni, ujumbe wa Jordan katika Umoja wa Mataifa umesisitiza katika taarifa yake kwamba, kuendelea hujuma na uvamizi wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa ni tishio kwa usalama na amani ya dunia.

Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zimekuwa zikikosolewa kutokana na kutochukua hatua za maana kwa ajili ya kukabiliana na hujuma na vitendo mbalimbali vya kinyama vya utawala haramu wa Kizayuni wea Isdrael dhidi ya Wapalestina.

/4008514

captcha