IQNA

Nchi za Ulaya zisifungamanishe maslahi yao utawala wa Israel unaosambaratika

20:07 - November 26, 2021
Habari ID: 3474601
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezinasihi nchi za Ulaya kutotoa mhanga maslahi yao ya kitaifa kwa manufaa na malengo haramu ya watawala wa Marekani na utawala haramu wa Israel.

Akizungumza katika hotuba za sala hiyo, Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabifard ameashiria kukaribia mazungumzo ya wawakilishi wa nchi za kundi la 4+1 huko mjini Vienna Austria na kusema: 'Leo hii kila mchambuzi na mjuzi wa masuala ya kisiasa anatambua vyema kuwa katika mustakbali wa karibu utawala ghasibu na wa Kizayuni wa Israel hautakuwepo tena katika eneo la Palestina na ulimwengu wa Kiislamu, hivyo nchi za Ulaya zisifungamanishe maslahi yao ya kitaifa na utawala huo ambao msingi wake umesambaratika na zikifanya hivyo hilo litakuwa ni kosa kubwa la kistratijia.'

Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran huku akifafanua kuwa maslahi ya nchi za Ulaya yanafungamana na maslahi ya mataifa ya Asia na hasa ya kusini magharibi mwa Asia amesema: Kama usingekuwa ni uwezo wa kisiasa na kielimu pamoja na mrengo wa mapambano katika eneo, nchi za Ulaya zingekabiliwa na hatari kubwa ya ukosefu wa usalama na ni mrengo huo wa mapambano ndio ulitokomeza genge la kigaidi na Daesh.'

Hujjatul Islam wal Muslimeen Abu Turabifard vilevile ameashiria matamshi ya karibuni ya Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alipokutana na wanafunzi na watu wenye vipawa maalumu vya kielimu nchini na kusema: 'Miongoni mwa mambo ya mfumo wa Kiislamu ambayo daima Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anayatilia mkazo ni kuimarishwa elimu na teknolojia nchini.'

Imamu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema nguvu inatokana na elimu na kwamba elimu ndiyo inayozalisha nguvu na kuongeza kuwa: 'Ikiwa elimu haitaambatanishwa na malezi na mafundisho ya mbinguni basi elimu hiyo itaelekeza kwenye ukoloni, ukandamizaji na ubeberu dhidi ya mataifa mengine.'

Hujjatul Islam Abu Turabifard amesema: 'Njia pekee ya kuiwezesha Iran kuwa na nguvu kubwa ni harakati ya kielimu, kufikia upeo wa elimu na kuwa miongoni mwa wazalishaji wakuu wa elimu na kwa maneno ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kubadilishwa Iran ya Kiislamu katika siku zijazo kuwa marejeo ya kielimu duniani.'

4016316/

captcha