IQNA

HAMAS yaunga mkono uamuzi wa Kuwait dhidi ya meli za Israel

18:38 - December 05, 2021
Habari ID: 3474643
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Palestina (HAMAS) imepongeza na kuunga mkono uamuzi wa serikali ya Kuwait wa kuzipiga marufuku meli za kibiashara zinazobeba bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel kutia nanga katika bandari za nchi hiyo.

Msemaji wa HAMAS, Hisham Qasim amesema katika taarifa kuwa, uamuzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera za Kuwait, juu ya kuwaunga mkono Wapalestina na njia yao ya haki.

Qasim amebainisha kuwa, hatua ya Kuwait mkabala wa meli za kibiashara za Israel inaenda sambamba pia na azimio la kuzitaka nchi za Kiarabu ziususie utawala wa Kizayuni wa Israel, lililopasishwa tangu mwaka 1950 na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League).

Jana Jumamosi, Rana Abdullah Al-Fares, Waziri wa Maslahi ya Umma wa Kuwait alitoa amri hiyo ambayo inapiga marufuku meli zinazosafirisha bidhaa za utawala haramu wa Israel kubeba au kushusha bidhaa hizo katika bandari za Kuwait. 

Kuwait haiutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel kama nchi na daima huitaja ardhi hizo kuwa ni Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

Kuwait ambayo iliwahi kushiriki katika vita dhidi ya utawala haramu wa Israel imepiga marufuku pia wakazi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kuingia katika ardhi ya nchi hiyo na inawazuia raia wake kushirikiana kwa njia yoyote na Wazayuni maghasibu.   

4018639

Kishikizo: hamas israel kuwait
captcha