IQNA

Washindi wa Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Misri watangazwa + Picha

21:14 - December 16, 2021
Habari ID: 3474681
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu Misri imetangaza washindi wa Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani yaliyofanyika wiki hii mjini Cairo.

Kategoria ya kwanza ya mashindano hayo ilikuwa ni kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu pamoja na qiraa ya Tajwidi pamoja na ufahamu wa maana ya aya. Kategoria hii ilikuwa ni maalumu kwa wazungumzao Kiarabu kama lugha ya kwanza na mshindi alikuwa ni Abdullah Ali Muhammad Muhammad wa Misri huku nafasi ya pili ikishikwa na Ayman Ahmad Mousa wa Misri akifuatiwa na Eman Gamal Farouh wa Misri pia na wa nne alikuwa ni Abdul Hamid Abdullah Omar wa Libya.

Kategoria ya pili ilikuwa ni kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na qiraa ya Tajwidi kwa wasiokuwa Waarabu ambapo nafasi ya kwanza imechukuliwa na Abubakr Tshamala wa Congo akifuatiwa na Mahmoud Ali Shanfo wa Comoro huku Abdul Rahman Saleh akichukua nafasi ya tatu naye Ali Attia Ibrahim wa Chad ameibuka wa nne huku nafasi ya tano ikishikwa na Drama Ismail wa Ivory Coast.

Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Misri yalianza Jumamosi na kumalizika Jumatano wiki hii mjini Cairo.

 

4021294

Kishikizo: misri mashindano qurani
captcha