Qarii kijana Mmisri Hani Al Azouni anasema Sura Maryam kwa sauti yenye mvuto na mtindo wa aina yake. Katika kilipu hii anasoma aya za 1-8 za Sura Maryam
- Kaf Ha Ya A'yn S'ad.
- Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
- Alipo mwita Mola wake Mlezi kwa siri.
- Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
- Na hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako.
- Atakaye nirithi mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Ewe Mola wangu Mlezi! Na umjaalie awe mwenye kuridhisha.
- (Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.
- Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimesha fikia ukongwe katika uzee?