IQNA

Darul Qur’an ya Iraq yaunga mkono harakati za Qur’ani Mali

13:01 - December 26, 2021
Habari ID: 3474724
TEHRAN (IQNA)- Kitengo cha Kimataifa cha Taasisi ya Darul Qur’an ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Hussein AS inaendeleza harakati zake za Qur’ani Tukufu nchini Mali.

Ali Abud al-Tani, mkuu wa harakati za Qur’ani barani Afrika katika taasisi hiyo amesema kati ya wanaofanya nchini Mali ni kuandaa warsha na vikao vya Qur’ani Tukufu.

Ameongeza kuwa kati ya warsha walizoandaa ni kuhusu kanuni za tajwid katika usomaji Qur’ani ambapo katika duru ya tano ya warsha hiyo wanafunzi 30 wa vyuo vikuu wameshiriki.

Aidha kila wiki huandaliwa vikao vya qiraa ya Qur’ani katika mabustani ya umma. Halikadhalika kuna mpango wa kuandaa kozi za Qur’ani Tukufu katika miji midogo iliyo mbali na miji mikubwa.

4023484

captcha