IQNA

Mahmoud Shahat Anwar amuiga baba yake katika usomaji Sura Al Fatiha + Video

TEHRAN (IQNA)- Qarii mashuhuri wa Misri Mahmoud Shahat Anwar hivi karibuni alisoma aya za Qur'ani akiiga mtindo wa marehemu baba yake.

Alishiriki katika kipindi cha televisheni ya En Nahar kwa mnasaba wa mwaka wa 14 wa babe yake ambapo alisoma Sura Al Fatiha akiwa anaiga mtindo wa usomaji wa baba yake, Marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar.

Sheikh Muhammad Shahat Anwar alizaliwa mwka 1950 katika kijiji cha Kafr el-Wazir katika jimbo la Dakahlia nchini na alianza kujifunza Qur'ani akiwa mtoto mdogo. Aliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8 na alipokuwa na umri wa miaka 10, alielekea katika kijiji cha Kafr el Maqam kujifunza Tajwidi kutoka kwa Ustadh Sayyid Ahmed Farahi.

Alifariki Januari 13 mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 57. Mwanae, Mahmoud ambaye sasa naye ni qarii mashuhuri alizaliwa mwaka 1984 na alihifadhi Qur'ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 12 sambamba na kupata maunfzo ya qiraa kutoka kwa baba yake. Amefanikiwa kushinda zawad kadhaa katika mashindano ya kimataifa. Amewahi kutembelea nchi kadhaa duniani kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu. Miongoni mwa nchi alizotembelea ni  Iraq, Iran, Qatar, UAE, Algeria, Syria, Pakistan, Afrika Kusini, Ugiriki, Uturuki na Ubelgiji.

 

4027517

Kishikizo: misri ، shahat ، anwar ، qurani ، shahat anwar