IQNA

Duru ya mchujo ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yaendelea

14:00 - January 13, 2022
Habari ID: 3474804
TEHRAN (IQNA)- Duru ya mchujo ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran imeanza Jumatano na itaendelea kwa muda wa siku nne.

Kwa mujibu wa taarifa mashindano hayo aghalabu yanafanyika kwa njia ya intaneti huku wasimamizi wakiwa katika Ukumbi wa Basirat mjini Tehran.

Katika duru hii ya ambayo inashirkisha wanaume, washiriki wanashindana katika qiraa ya Qur'ani Tukufu na Tarteel.

Halikadhalika duru hii itakuwa na kitengo kile cha kawaida na kisha mashindano maalumu ya wanafunzi wa shule na yale ya wenye uleamvu wa macho. Duru ya mchujo ya wanawake ilikamilika Jumatatu.

Washiriki ambayo wanajumuisha waliohifadhi Qur'ani na wasomaji kutoka nchi 69 wanashiriki katika mashindano ya kimataifa ya mwaka huu.

Duru ya mchujo ya mashindano inafanyika kwa njia ya intaneti ambapo watakaofaulu watashiriki fainali katika mashindano yatakayofanyika nchini Iran baadaye mwezi Machi mwaka huu na hilo litategemea hali ya janga la COVID-19 duniani.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashidano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran kila mwaka.

4028013

captcha