IQNA

Maafisa wa Polisi Nigeria warejea baada ya kutoweka kufuatia hujuma ya magaidi wa Daesh

23:25 - January 15, 2022
Habari ID: 3474810
TEHRAN (IQNA)- Maafisa tisa wakufunzi wa polisi Nigeria ambao ni wahadhiri wamerejea baada ya kutoweka kufuatia hujuma dhidi ya kambi yao iliyotekelezwa na kundi la igaidi linalofungamana na Daesh au ISIS.

Taarifa zinasema kuwa kundi la kigaidi la ISIS Mkoa wa Afrika Kaskazini (ISWAP) wiki iliyopita lilitekeleza shambulizi  hilo Alhamisi dhidi ya Chuo cha Mafunzo ya Poisi cha Limankara jimboni Borno.

Afisa mwandamizi wa polisi amesema maafisa hao, ambao inaamnika walikuwa wametekewa nyara na magaidi walirejea kambini leo Jumamosi.

Hayo yanajiri wakati ambao, majambazi waliokuwa wamejizatiti kwa silaha juzu wametekekeleza mashambulizi katika majimbo ya Plateau na Niger nchini Nigeria na kuuawa raia wasiopungua 52.

Mashambulizi hayo yamejiri wiki moja baada ya zaidi ya watu wengine 200 kuuawa katika hujuma ya majambazi katika jimbo la Zamfara, kaskazini magahribi mwa Nigeria.

Taarifa zinasema watu 18 wameuawa katika shambulizi dhidi ya jamii ya Ncha, katika sehemu ya Bassa, jimbo la Plateau, huku watu wengine 34 wakiuawa katika sehemu za Nakuna na Wurukuchi, jimbo la Niger.

Tukio katika jimbo la Niger limeonekana kuwa la kulipiza kisasi, baada ya kutokea mauaji wiki chache zilizopita pale wapiganaji wa kijamii katika eneo hilo kuua watu kadhaa waliokuwa wamejihami kwa silaha na waliokuwa wanashutumiwa kwa kuwahangaisha raia.

Wiki iliyopita Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliahidi kuwa serikali haitalegea katika vita vyake dhidi ya majambazi wanaowahangaisha wananchi.

Maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Nigeria yamekuwa yakishuhudia ongezeko kubwa la vitendo vya uhalifu huku serikali ikiwa mbioni kurejesha amani bila mafanikio. Mwaka jana majambazi waliwateka mamia ya watoto wa shule na kudai vikomboleo kabla ya kuwaachilia huru. Idadi kubwa ya wanafunzi bado wako mikononi mwa watekaji nyara.

Wiki iliyopita Jeshi la Nigeria lilitangaza kuwa tokea mwezi Mei mwaka jana, limewaua majambazi 537 na kuwakamata wengine 374 huku raia 452 waliokuwa wametekwa nyara wakiachiliwa huru.

3477384

Kishikizo: nigeria magaidi iswap
captcha