IQNA

Picha za Satalaiti za Mashambulio ya Wayamen dhidi ya UAE

16:04 - January 18, 2022
Habari ID: 3474823
TEHRAN (IQNA)- Katika hali ambayo mashirika ya mafuta ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) bado hayajatangaza hasara yalizopata kufuatia mashambulio ya ulipizaji kisasi yaliyotekeleza na Jeshi la Yemen, lakini picha za satalaiti zinaonyesha uharibifu mkubwa uliofanyika.

Televisheni ya Al Alam imeripoti kuwa, picha za satalaiti zinaonyesha hasara kubwa iliyopatikana katika vituo vya kusafisha mafuta ghafu ya petroli nchini UAE. Jeshi la Yemen limetangaza rasmi kuwa limehusika na mashambulio hayo ya jana ikiwa ni sehemu ya kulipiza kisasi jinai zinazofanywa na UAE ambayo inashirikiana na Saudi Arabia katika vita dhidi ya Yemen.

Jeshi la Yemen kwa kushirikiana na Ansarullah jana limeshambulia ndani kabisa ya ardhi ya UAE kwa kutumia ndege 20 zisizo na rubani na makombora 10 ya balestiki. Kwa uchache watu watatu wameuawa na wengine 6 kujeruhiwa katika shambulio hilo la kulipiza kisasi.

Aidha ndani ya Yemen, ndege ya mizigo ya kijeshi mali ya jeshi la Imarati imelengwa katika Uwanja wa Ndege wa Ataq katika mkoa wa Shab'wah kusini mwa Yemen. Mashambulio hayo ya Wayamen dhidi ya Imarati yanaweza kutathminiwa katika nukta kadhaa.

Indhari ya awali

Mosi; mashambulio haya yamefanyika baada ya maonyo na indhari kadhaa za Wayamen dhidi ya UAE. Licha ya kuwa serikali ya imarati Februaria mwaka 2020 ilitangaza kuondoa askari wake huko Yemen, lakini nchi hiyo iliendeleza uingiliaji wake wa kisiasa katika masuala ya ndani ya Yemen na vilivile katika miezi ya hivi karibuni imeongeza kasi ya harakati zake za kijasusi katika nchi hiyo.

Ni kwa msingi huo ndio maana viongozi wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen wakaionya UAE kuhusiana na matokeo mabaya ya kuendeleza siasa zake hizo. Muhammad al-Bukhaiti, Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Ansarullah ya Yemen hivi karibuni aliionya UAE na kuitaka iachane na siasa zake chafu za kuzusha machafuko na mizozo kwani kama mwenendo huo utaendelea, basi Yemen italazimika kushambulia ndani ya ardhi ya nchi hiyo.

عکس‌های ماهواره‌ای از حمله به سایت نفتی ابوظبی

Vituo vya mafuta vya UAE kabla ya kushambuliwa. Picha iliyotangulia inaonyesha baada ya kushambuliwa

Kwa muktadha huo, mashambulio ya jana yalikuwa ni kutekeleza kivitendo indhari na onyo la hapo kabla ambalo UAE ilipatiwa na Harakati ya Wananchi ya Ansarullah ya Yemen. Muhammad Abdul-Salam, msemaji wa Ansarullah ya Yemen na Mkuu wa Timu ya Mazungumzo ya Sana’a naye akitoa radiamali yake kwa operesheni ya jana dhidi ya Imarati ametangaza kuwa, nchi ndogo katika eneo ambayo inajitolea roho yake kwa ajili ya kuihudumia Marekani na utawala haramu wa Israel imedai kwamba, imeondoka nchini Yemen, lakini hivi karibuni imethibiti kinyume kabisa na madai ya taifa hilo.

Utawala wa Israel

Pili; katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Umoja wa Falme za Kiarabu umeufungulia njia utawala haramu wa Israel huko kusini mwa Yemen ambapo hivi karibuni kumeanza kujengwa kambi ya kijeshi nchini Yemen. Duru za Yemen zimetangaza kuwa, kambi hiyo ya kijeshi mali ya Israel inatarajiwa kujengwa katika Kisiwa cha Abdelkuri kilichoko katika majimui ya visiwa vya Socotra. Imarati imeanza kujenga kambi hiyo ya kijeshi kwa uratibu na Shirika la Kijasusi la utawala huo ghasibu.

Inaonekana kuwa, dhana ya UAE ni hii kwamba, kupitia kivuli cha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala vamizi wa Israel itaweza kwa urahisi kusukuma mbele gurudumu la siasa zake za uingiliaji masuala ya ndani nchini Yemen. Hivi karibuni Wayamen waliikamata meli ya Imarati katika maji ya Yemen iliyokuwa imesheheni silaha. Shambulio la jana katika ardhi ya Imarati linahesabiwa kuwa jibu kali la Wayamen la kupinga ushirikiano wa Abu Dhabi na utawala haramu wa Israel kusini mwa Yemen.

Maeneo ya kiuchumi

Tatu; katika mashambulio ya jana miongoni mwa maeneo yaliyolengwa ni eneo la viwanda na Uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi ambayo yalishambuliwa kwa ndege zisizo na rubani pamoja na makombora ya balestiki. Kimsingi ni kuwa, Wayamen wamefikia utambuzi huu kwamba, uchumi wa nchi yao ni wenye kudhurika mno mkabala wa kila aina ya ukosefu wa usalama.

Ni kwa msingi huo ndio maana wamechukua hatua ya kuyalenga maeneo ya kiuchumi ya UAE. Kanali ya Televisheni ya Russia al-Yaum sambamba na kuashiria katika ripoti yake umuhimu wa eneo la kiviwanda la al-Misfah huko Abu Dhabi imeripoti kwamba: Eneo hilo linapatikana kusini mwa Abu Dhabi na linahesabiwa kuwa moja ya maeneo muhimu kabisa ya kiuchumi nchini UAE. Akthari ya mashirika ya kiviwanda na utengenezaji magari yanapatikana katika eneo hilo ambapo mbali na bandari ya kale kabisa ya nchi hiyo kupatikana katika eneo hilo, kuna maduka makubwa ya uuzaji magari pamoja na vituo vya kukarabati magari na kuhifadhia magari yenye nembo za kimataifa kama Bentley, Porsche na Volkswagen.

Uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi nao una umuhimu wa kistratejia kwa nchi ya Imarati. Kulengwa kwa mashambulio maeneo hayo na Wayamen ni indhari na onyo la kivitendo kwa Imarati. Akizungumza na Kanali ya Televisheni ya al-Jazeera ya Qatar, Muhammad al-Bukhaiti, Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Ansarullah ya Yemen  ametangaza kuwa, kama Imarati itaendele na mashambulio yake dhidi ya Yemen, basi ijiandae kukabiliwa na mashambulio makubwa na ya kuumiza zaidi.

4029478

captcha