IQNA

Walowezi wa Kizayuni wameng'oa mizeituni 400 ya Wapalestina

17:27 - January 22, 2022
Habari ID: 3474838
TEHRAN (IQNA)- Walowezi wa Kizayuni watenda jinai wameng'oa miembe 400 ya Wapalestina katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel katika Ukingo wa Magharibu wa Mto Jordan.

Taarifa zinasema jinai hiyo imejiri Ijumaa katika kijiji cha Deir Sharaf ambapo Wazayuni watenda jinai walihujumu shamba ijulikanayo kama Al Harayek na kuanza kung'oa na kukata mizeituni.

Wamiliki halali wa ardhi hiyo wametambuliwa kuwa ni Abdul Rahim, Abdul Hamid na Ghazi Antari ambao wote ni wanakijiji wa Deir Sharaf.

Wazayuni hao wameendeleza jinai hiyo kwa kung'oa mizeituni 90 ya wakulima Wapalestina katika kijiji cha Salfti cha Ukingo wa Magharibi.

Walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakikata mizeituni na kuharibu mashamba ya Wapalestina mara kwa mara kinyume cha sheria za kimataifa. Jinai hizo za Wazayuni huungwa mkono na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa muda mrefu sasa utawala wa Kizayuni umekuwa ukiteka ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kuvuruga muundo wa kijiografia na kijamii katika maeneo ya Wapalestina kwa uungaji mkono wa kila upande wa Marekani.

Utawala wa Kizayuni unaendeleza ujenzi huo haramu wa vitongoji katika ardhi za Palestina huku ukipuuza takwa la jamii ya kimataifa la kusimamisha ujenzi huo kwa kukingiwa kifua na Marekani. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ujenzi wa vitongoji vyote vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina ni kinyume cha sheria.  

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

3477481

captcha