Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Palestina imelaani vikali hujuma hiyo na kuotaja kuwa katika njama za utawala ghasibu wa Israel za kuudhibiti msikiti huo na kuubadilisha kuwa hekalu la Wazayuni.
Msikiti wa Ibrahim AS ambao ni eneo takatifu kwa Waislamu na Mayahudi ni Haram Takatifu na uko katika kitongoji cha kale cha Al Khalil (Hebron) kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, ndani ya msikiti huo kuna kaburi la Nabii Ibrahim AS na mkewe Sarah na vile vile makaburi ya Manabii Is-haq na Yaaqub AS na ya wake zao.
Itakumbukuwa kuwa mnamo mwezi Julai mwaka 2017, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitangaza kuwa mji wa Al Khalil ulioko Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan ambao ni moja ya turathi za kimataifa unakabiliwa na hatari kutokana na sera haribifu za utawala wa Kizayuni.