IQNA

Vita dhidi ya Yemen

Marekani yawataka raia wake UAE wachukue tahadhari

17:05 - January 25, 2022
Habari ID: 3474852
TEHRAN (IQNA)- Ubalozi wa Marekani katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umetoa onyo la usalama la hali ya juu kwa Wamarekani wanaoishi huko Imarati kufuatia mashambulizi ya makombora ya jeshi la Yemen na wapiganaji wa Ansarullah huko Abu Dhabi.

Kufuatia kushadidi mashambulizi ya muungano vamizi wa Saudia katika maeneo mbalimbali ya Yemen na onyo la maafisa wa Sanaa kwa tawala za Saudi Arabia na Imarati zinazozikalia kwa mabavu ardhi ya Yemen, vyanzo vya habari vimeripoti mapema leo Jumatatu kwamba milipuko minne imetokea katika mji mkuu wa Imarati, Abu Dhabi na kusini mwa Saudia. 

Baada ya milipuko iliyotokea Abu Dhabi, ubalozi wa Marekani umetoa onyo la usalama kwa Wamarekani wanaoishi katika UAE, na kusema: "Onyo hili linajumuisha maagizo ya jinsi ya kukabiliana na mashambulizi ya makombora."

Milio ya ving'ora ilisikika kote katika mji wa Abu Dhabi baada ya jeshi la Yemen kuvurumisha makombora kadhaa mapema leo katika mji huo. Wakati huo huo Saudi Arabia imetangaza kuwa kombora la balestiki la Jeshi la Yemen limepiga eneo la Gizan huko kusini mwa nchi hiyo. 

Wakati huo huo Msemaji wa kamandi kuu ya jeshi la kigaidi la Marekani CENTCOM amekiri kuwa, askari wa jeshi hilo walikimbilia mafichoni kwa kuhofia uwezekano wa jeshi la Yemen kuishambulia tena Imarati, kufuatia shambulio la makombora na ndege zisizo na rubani za jeshi hilo katika mji wa Abu Dhabi. 

Jumatatu iliyopita, vikosi vya jeshi la Yemen vilishambulia kwa makombora na droni viwanja vya ndege vya Dubai na Abu Dhabi baada ya Yemen kuionya mara kadhaa Imarati kwamba iache kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Imarati ni mshirika mkuu wa Saudi Arabia katika hujuma na mashambulizi yanayoendelewa kufanywa na nchi hizo mbili na waitifaki wao dhidi ya taifa la Yemen. 

Juzi Msemaji wa Jeshi la Yemen aliyashauri makampuni ya kigeni ya uwekezaji kuondoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) akisisitzia kuwa,  makampuni ya kigeni yaliyowekeza katika nchi hiyo ndogo hayatakuwa salama.

Matamshi hayo ya msemaji wa Jeshi la Yemen yametolewa kufutia hujuma kubwa ya ndege za kivita za Saudi Arabia iliyolenga makazi na raia na jela la mkoa wa Sa'ada. Watu wasiopungua 80 wameuawa katika mashambulizi hayo ya kinyama na wengine karibu 150 wamejeruhiwa. 

4031048/

captcha