IQNA

22:05 - May 11, 2022
Habari ID: 3475236
TEHRAN (IQNA)- Wakazi wa kijiji cha Al-A'aija nchini Algeria wamemkaribisah kwa furaha Faisal Hajjaj, mkazi wa kijiji hicho ambaye aliibuka wa kwanza kitaifa katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya watoto.

Wanakijiji wanasema wanahisi fahari kubwa kuwa Faisla ameweza kupata mafanikio hayo makubwa.

Faisal anasema anamshukuru Mwenyezi Mungu SWT kwa kumuwezesha kupata mafanikio hayo. Aidha wamewashukuru waalimu wake wa Qur'ani ambao wamechangia pakubwa katika mafanikio yake. Halikadhalika Faisal ametoa shukrani maalumu kwa wazazi wake ambao walimuandalia mazingira sambamba na kumpa himaya na motisha katika jitihada zake za kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yalifanyika hivi karibuni na kuwaleta paoja watoto na mabarobaro kutoka maeneo mbali mbali ya Algeria.

4056158

Kishikizo: algeria ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: