IQNA

Ayatullah Fateminia mwanazuoni maarufu wa akhlaqi za Kiislamu Iran aaga dunia

12:12 - May 16, 2022
Habari ID: 3475257
TEHRAN (IQNA)- Ayatullah Sayyid Abdullah Fateminia, mwanazuoni maarufu wa akhlaqi za Kiislamu ameaga dunia.

Alirejea kwa Mola Wake Jumatatu asubuhi akiwa na umri wa miaka 76 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mbali na kuhubiti na kutoa mihadhara pia alikuwa mtafiti aliyebobea katika sekta za Hadithi, mashari ya kiarabi, akhlaqi, irfani na pia aliandika tafsiri za Nahj-ul-Balagha na Sahifa Sajjadiya.

Ayatullah Fateminia alikuwa maarufu kutokana na mihadhara yake ambayo ilikuwa iinarushwa mara kwa mara katika televisheni ya Iran.

Alizaliwa mwaka 1946 katika mji wa Tabriz, kaskazini-magharibi mwa Iran. Akiwa mtoto alijifunza dini na sayansi kutoka kwa baba yake, Ayatullah Sayyid Ismail Asfiaei Shendabadi na kisha baada ya hapo kwa muda wa miaka 30 alikuwa mwanafunzi wa Allamah Mostafavi ambaye naye alikuwa mwanafunzi wa Ali Qadhi Tabatabai.

Ayatullah Tabatabai pia alijiunga na vyuo vya kidini na kuendeleza masomo yake. Kati ya waalumu wake wengine tunaweza kuwataja wanazuoni maarufu wa Kiislamu kama vile Allamah Tabatabaei, Sayyid Mohammad Hassan Elahi Tabatabaei, Muhammad Taqi Amoli, na Sayyid Reza Bahaadini.

4057274

captcha