IQNA

Hali nchini Afghanistan

Watu 16 wauawa katika hujuma za kigaidi nchini Afghanistan

16:43 - May 26, 2022
Habari ID: 3475298
TEHRAN (IQNA)- Maafisa wa Afghanistan wanasema idadi ya watu waliouwawa kufuatia mashambulizi manne ya mabomu yaliyofanyika kwenye basi dogo na msikitini nchini humo imefikia watu 16.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh wamedai kuhusika na baadhi ya mashambulizi hayo. Jana kiasi watu 10 waliuwawa katika mashambulizi matatu ya mabomu yaliyotegwa kwenye mabasi mawili madogo na kuripuka katika mji wa kaskazini mwa nchi wa Mazar-i-Sharif na watu wengine 15 walijeruhiwa kwa mujibu wa polisi na madaktari.

Jumatano msemaji wa polisi mjini Kabul, Khalid Zadran ameandika ujumbe kupitia mtandao wa Tweeter uliosema watu sita wameuwawa katika shambulizi la bomu dhidi ya Msikiti wa Hazrat Zakaria  na wengine 18 wameruhiwa. Amesema hujuma hiyo ilijiri wakati waumini wakiwa ndani ya msikiti wakati wa Sala ya Magharibi.

Mashambulio ya kigaidi na miripuko kwenye maeneo tofauti ya Afghanistan inaonesha kuwa, serikali ya Taliban imeshindwa kulinda usalama wa wananchi. Aidha inadokezwa kuwa Marekani inalitumia kundi la kigaidi la ISIS au Daesh kutekeleza hujuma dhidi ya watu wa Afghansitan.

4059722

captcha