IQNA

Hatua za usalama zimechukuliwa katika misikiti nchini Ghana

17:06 - May 26, 2022
Habari ID: 3475300
TEHRAN (IQNA)- Kufuatia tahadhari kutoka kwa serikali ya Ghana kuhusu uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi, ulinzi umeimarishwa misikitini kwa amri ya kiongozi wa Kiislamu wa nchi hiyo, Mallam Othman Nuhu Sharubutu.

Msemaji wa Mallam Nuhu Sharubutu amesema kiongozi huyo ana wasiwasi na hali ilivyo nchini humo na kuitaka jamii ya Kiislamu kuchukua hatua kali ili kuzuia mashambulizi.

Aidha ameutaka ulimwengu wa Kiislamu kuwafichua watu au watu wenye misimamo mikali wanaotaka kudhuru jamii.

Msemaji wa kiongozi wa Kiislamu wa Ghana alisema: "Tumeziomba kamati za usimamizi wa misikiti kufunga kamera za CCTV. Hii ni hatua ambayo haijawahi kuchukuliwa. Pia tunawataka kutumia huduma za makampuni binafsi ya usalama na kufuatilia watu wanaoshukiwa kuwa ni wahalifu."

Aliongeza: "La muhimu zaidi, tunatoa wito kwa umma wa Kiislamu na misikiti kusaidia kutambua watu wenye harakati zisizo za kawaida."

Hapo awali, Eduardo Coco Asumani, naibu mratibu wa usalama wa Ghana, alielezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa ugaidi katika eneo la Afrika Magharibi.

Kulingana na afisa wa serikali, zaidi ya mashambulizi 340 katika robo ya kwanza ya mwaka katika eneo hilo yanaashiria kuwa eneo hilo limekuwa kitovu cha ugaidi hivyo ufahamu wa umma kuhusu usalama ni muhimu.

Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Ghana imezindua kampeni ya "Sema Unachokiona" ili kuwahimiza raia wa Ghana kuongeza usalama kwa kutoa taarifa kwa maafisa wa usalama."

4059565

captcha