Kwa mujibu wa taarifa, wavulana na wasichana 8,695 wa Uturuki wamefanikiwa kuhifadhi Qur'ani kikamilifu katika mwaka wa masomo wa 2021-22.
Wamepokea vyeti vya kuhifadhi Qur'ani kutoka Idara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki (Diyanet) baada ya kutimiza vigezo vyote. Mwaka jana wanafunzi wengine 73,000 walishiriki katika kozi za kuhifdhi Qur'ani kote Uturuki katika mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa Diyanet, jumla ya watu zaidi ya laki mbili Uturuki wana vyeti vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Kuna misikiti takribani 90,000 Uturuki na kila mwaka huandaa masomo maalumu ya kuhifadhi Qur'ani, Tafsiri na masomo mengine ya Kiislamu.