IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tanzania yanafanyika Alhamisi

13:08 - August 10, 2022
Habari ID: 3475601
TEHRAN (IQNA) - Hatua ya mwisho ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu itafanyika jijini Dar es-Salaam, jiji kubwa zaidi la Tanzania, siku ya Alhamisi.

Ni toleo la tatu la mashindano hayo, ambay huandaliwa kila mwaka na Wakfu wa Maulamaa wa Afrika wa  Mfalme Mohammed VI  wa Morocco.

Kutakuwa na wagombea 88 kutoka nchi 34 wanaoshindana katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani Tukufu na halikadhalika Tajweed na Tarteel.

Msikiti wa Mohammed VI jijini Dar es-Salaam utakuwa mwenyeji wa toleo hili la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu.

Washiriki wanawakilisha matawi ya Wakfu wa Maulamaa wa Afrika wa  Mfalme Mohammed VI  katika nchi tofautiza Afrika

Taasisi hiyo pia itaandaa maonyesho maalumu ya Qur'ani Tukufu pembezoni mwa mashindano hayo ambayo yataonyesha historia, mapambano, na aina za kisanii za nakala za Qur'ani nchini Morocco.

Katika onyesho kutakuwa na nakala za Qur’ani Tukufu katika enzi tofauti, zikiwemo zile zilizochapishwa na Wizara ya Wakfu ya Morocco na Taasisi ya Uchapishaji Qur’ani ya Mohammed VI.

Wakfu wa Maulamaa wa Afrika wa  Mfalme Mohammed VI  , kwa mujibu wa waanzilishi wake, ni taasisi ya kidini ya Kiislamu inayotaka kuzuia itikadi kali na kupiga vita malumbano ya kimadhehebu ndani ya Uislamu.

Lengo la msingi ni kuunganisha na kuratibu juhudi za wasomi  wa Kiislamu kutoka Morocco na nchi nyingine za Afrika ili kuunganisha maadili ya Kiislamu ya kustahamiliana.

Pia wakfu huo unalenga kuwezesha hatua za kiakili, kisayansi na kitamaduni kwa kuwaleta pamoja na wasomi Waislamu kutoka duniani kote ili kuhimiza uanzishwaji wa vituo vya kidini, kisayansi na kitamaduni na kufanya kazi kuelekea kufufua urithi wa pamoja wa kitamaduni wa Kiafrika, wa Kiislamu.

captcha