IQNA

Kususia Israel

Oman yasema haitafuata mkondo wa Saudia katika kuruhusu ndege za Israel zitumie anga yake

22:39 - August 11, 2022
Habari ID: 3475608
TEHRAN(IQNA)- Oman imekataa kuidhinisha ndege za utawala wa haramu wa Israel kuruka katika anga yake, ikionekana kujiepusha kufuata nyayo za Saudi Arabia za kujikurubisha wazi wazi na utawala huo haramu.

Televisheni ya RT iliripoti Jumatano kwamba Oman bado haijatoa ridhaa yake ya kufungua anga zake kwa mashirika ya ndege ya Israel.

Safari za ndege kupitia anga ya Oman zinaweza kutoa njia fupi za anga kwa ndege za Israel hadi Mashariki ya Mbali, kulingana na ripoti hiyo.

"Idhini ya Oman ni muhimu sana na muhimu kwa Israeli kwa sababu, bila ridhaa yake, ndege zinazotumia anga ya Saudi Arabia haziwezi kusafiri hadi Bahari ya Hindi na kisha kwenda maeneo mbalimbali ya Mashariki," ripoti hiyo imesema.

Imeongeza kuwa iwapo Oman haitafungua anga yake kwa Israel, ndege"lazima zipite kwenye anga ya Yemen ili kuruka kuelekea mashariki jambo ambalo haliwezekani, kutokana na vita vya Saudia dhidi ya Yemen na ukweli kwamba Tel Aviv na Sana'a hazina uhusiano wowote wa kidiplomasia."

Taarifa hiyo imesema ingawa Oman ina uhusiano usio wa wazi na Israel, lakini haijaruhusu ndege ya Israel kutumia anga yake.

Utawala haramu wa Israel umeongeza juhudi zake zinazoungwa mkono na Marekani za kuanzisha uhusiano wa wazi na wa kawaida na Oman, miongoni mwa nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

Mwezi uliopita, Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Saudia (GACA) ilisema katika taarifa kwamba anga ya nchi hiyo sasa iko wazi kwa mashirika yote ya ndege, ikiwa ni pamoja na yale ya Israel, kufuatia safari ya Rais wa Marekani Joe Biden katika ufalme huo.

Akizungumza na gazeti la Kifaransa la Le Figaro mwishoni mwa mwezi wa Mei, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr al-Busaidi alifafanua kuwa Oman haitakuwa na uhusiano wa kawaida na wa wazi na Israel hadi suala la Palestina litatuliwe.

"Oman haitajiunga na nchi za Ghuba ya Uajemi ambazo zimetangaza kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa  Israel," alisema, na kuongeza kuwa Oman "inafadhilisha mipango inayounga mkono watu wa Palestina."

3480050

3480050

captcha