IQNA

Waliowachache

Qur’ani Tukufu imetumwa kwa wanadamu wote, sio Waislamu pekee

23:08 - August 12, 2022
Habari ID: 3475613
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Pakistan wa Masuala ya Kidini na Upatanifu wa Dini Mbalimbali amesisitiza kwamba Qur’ani Tukufu iliteremshwa kwa ajili ya wanadamu wote, si kwa ajili ya Waislamu pekee.

Akinukuu aya ya Qur'ani Tukufu wakati wa hafla iliyoandaliwa kuhusiana na Siku ya Wachache Kitaifa huko Islamabad Alhamisi, Mufti Abdul Shakoor alisema kuwa Mwenyezi Mungu SWT amezungumza na wanadamu wote katika Surah Naas, na Yeye ndiye Mungu wa walimwengu wote, kwa mtazamo wa Qur’ani Tukufu.

Waziri huyo alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mungu wa jumuiya zote, zikiwemo za Kihindu, Kikristo, Kalasinga na nyinginezo.

Alisema kuwa kama wanadamu wote ni wenye kuheshimika; kwa hivyo wanapaswa kueneza upendo na amani miongoni mwao.

Alisema kuwa hakuna dhana ya kusilimu kwa lazima katika Uislamu, kwani ni dhambi kubwa kulazimisha kwa kuzingatia mafundisho ya dini hii tukufu.

Akitoa mshikamano na jumuiya za walio wachache Pakistan, aliwahakikishia uungaji mkono wake wa dhati kwao na kusema kwamba ikiwa atapata kuwatumikia watu kama waziri wa masuala ya kidini kwa muda mrefu, ataendeleza mapambano yake ya kutetea haki za kisheria za walio wachache.

Alisema zaidi kwamba walilazimika kutoa huduma za kimsingi haswa kwa watu wa jamii za wachache ambao walikuwa wakiishi katika maeneo ya mbali ya nchi.

3480057

captcha