IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Austria ingageuka kuwa ngome ya wenye chuki dhidi ya Uislamu

18:38 - August 14, 2022
Habari ID: 3475619
Austria ni maarufu kwa usanifu majengo mzuri na sanaa, hata hivyo, cha kusikitisha ni kwamba, nchi hii sasa imejijengea sifa nyingine katika miaka ya hivi karibuni: ile ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Waislamu waliowachache.

Kulingana na data iliyotolewa Juni 2022, zaidi ya matukio 1000 ya chuki dhidi ya Uislamu yaliripotiwa mwaka uliopita; ongezeko la kushangaza, ambalo limekua mwaka hadi mwaka.

Utafiti kuhusu uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu nchini Austria umegundua kwamba idadi kubwa ya mashambulizi hayo, ambayo hufanyika ni wanaume wakiwalenga wanawake: huku asilimia 69 ya wahasiriwa wakiwa ni wanawake, wengi wao wakiwa wamevaa hijabu. Hata hivyo, sio uhalifu wa mitaani pekee unaotekelezwa, ambao unawalenga Waislamu.

Mvutano mkali wa 2021 ulidaiwa kuchochewa na serikali yenye utata iliyotekelezwa "Ramani ya Uislamu," iliyoanzishwa na mamlaka ili kufanya upelekelezi na ujasusi katika misikiti yote kote Austria. Wakosoaji wanaamini kuwa sera hii ilichangia kuchochea  kuenea kwa uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu.

Mnamo Novemba 2020, mamlaka ya Austria ilizindua Oparesheni Luxor, ambayo ilishuhudia nyumba na ofisi za mashirika ya kutoa misaada ya Kiislamu na wanaharakati zikivamiwa kama sehemu ya kile kinachoitwa vita dhidi ya "Uislamu wa kisiasa."

Lakini wakosoaji wanasema  mafanikio yake pekee ni kuwadhalilisha Waislamu na kuzidisha hofu ya umma dhidi ya Uislamu. Kuongezeka kwa hofu karibu kunasababisha chuki zaidi.

3480084

captcha