IQNA

Fikra za Kiislamu

Kusema uongo huondoa uaminifu

22:27 - September 22, 2022
Habari ID: 3475823
TEHRAN (IQNA) – Mwanadamu kiuhalisia hufuata ukweli. Anataka kusikia, kuona na kusema ukweli, lakini wakati mwingine husahau asili yake na kwa kusema uwongo o na hivyhuacha ukweli.

Kwa hivyo, hakuna shaka kuwa uongo unapingana na asili na ukweli wa mwanadamu.

Kuna misukumo tofauti ya kusema uwongo lakini cha muhimu ni kutokuzoea kitu ambacho ni kinyume na nafsi na uhalisia wa kuwa binadamu na kupelekea mtu kufikia mahali anapoteza thamani na hadhi yake.

Qur’ani Tukufu inasema kusema uwongo na jambo ambalo mtu haliamini ni moja  ya sifa ya wanafiki: “ Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo." (Surah Al-Munafiqun, Aya ya 1)

Qur’ani Tukufu inamtaja Shetani kama chimbuko la uwongo na inaonya kwamba Shetani huwahimiza watu kusema uwongo na hutumia uwongo kufikia malengo yake juu ya kudanganya watu.

“Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani? Wanamjia kila mwongo mwingi wa dhambi." (Sura Ash-Shu’ara, Aya ya 221-222)

Uongo, kama uovu wa kimaadili na dhambi ya kibinafsi na ya kijamii ina matokeo mengi, muhimu zaidi ambayo katika nyanja ya kijamii ni kuondoa uaminifu kati ya mtu na mwingine katika jamii.

Uongo unapoenezwa katika jamii, watu hawawezi kuaminiana na kila mtu anasema nini katika eneo lolote.

Anayepata madhara zaidi kutokana na kusema uwongo ni mwongo mwenyewe. Uongo ni kama mchwa ndani ya uwepo wa mtu ambaye polepole huharibu tabia, sifa na hadhi yake.

Na akasema mtu mmoja Muumini, aliye kuwa mmoja katika watu wa Firauni aliye ficha Imani yake: Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu? Na hali naye amekujieni na hoja zilizo wazi? Na akiwa yeye mwongo basi uwongo wake ni juu yake mwenyewe, na akiwa mkweli yatakufikieni baadhi ya hayo anayo kuahidini. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo mkubwa. (Surah Ghafir, Aya ya 28)

captcha