IQNA

Mapambano dhidi ya Israel

Mwanachuoni wa Lebanon akosoa tawala za Kiarabu zilizoanzisha uhusiano na Israel

17:49 - October 05, 2022
Habari ID: 3475882
TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni mmoja wa ngazi za juu wa Lebanon amelaani baadhi ya tawala za Kiarabu kwa kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel, akisema makubaliano yao na Wazayuni hayana thamani yoyote ya kistratijia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama (Mapambano ya Kiislamu) Sheikh Maher Hammoud amesema tawala za aina hiyo zimewekwa na Marekani na Uingereza katika eneo ili kuhudumia mradi wa Wazayuni wa kikoloni.

Amesema hata hivyo hatua zao hazitabadilisha ukweli wowote kwani Wapalestina wataendelea kutetea ardhi zao na matakatifu yao.

Aliongeza kuwa mataifa yote ya Kiarabu yataendelea kuunga mkono ukombozi wa Palestina.

Sheikh Hamoud aidha amebainisha kuwa, Mhimili wa Muqawama unaendelea kuunga mkono mapambano ya Wapalestina licha ya mashinikizo yote ya madola yenye kiburi.

Khatibu huyo mkuu amepongeza ushujaa wa Wapalestina wanaoulinda Msikiti wa Al-Aqswa huko al-Quds (Jerusalem) dhidi ya wanajeshi wa utawala bandia wa Israel unaokali ardhi za Palestina kwa mabavu.

Kauli yake inakuja wakati hivi karibuni vikosi vya Israel vimekuwa vikiendesha mashambulizi na mauaji ya usiku kucha huko al-Quds na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Zaidi ya Wapalestina 150 wameuawa na wanajeshi wa Israel katika maeneo yanayokaliwa na Israel tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakiwemo 51 katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa wakati wa mashambulizi ya siku tatu ya Israel mwezi Agosti.

4089643

captcha