IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje /31

Waislamu washauri dhidi ya kuiga kipofu

17:50 - October 13, 2022
Habari ID: 3475923
TEHRAN (IQNA) - Mwenyezi Mungu SWT katika Qur'ani Tukufu amewakataza watu kuiga kipofu au au kufuata bila kuuliza.

Mtazamo huu wa Qur'ani Tukufu  umefungua njia ya kuwawezesha Waislamu kustawi na kunawiri katika sekta mbali mbali.

Hapo zamani za kale, kuwaiga na kuwafuata baba na wahenga ilikuwa jambo la kawaida katika jamii. Uigaji huo wa upofu ambao ni wa uharibifu pia unaonekana katika jamii za kisasa.

Uigaji kama huu ambao haufai huwa na matokeo mawili ya kutisha: Kwanza, unaficha ukweli katikak maisha ya binadamu na, pili, unazuia njia ya ukuaji, maendeleo mbali na kumzuia mwanadamu kubadilisha mwelekeo.

Aya ya 170 ya Sura Al-Baqarah ni miongoni mwa aya za Quran zinazoharamisha kuiga bila ya kufikiri: “ Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?

Ayatullah Nasser Makarem Shirazi katika Tafsiri yake ya Qur'ani Tukufu ya Nemuneh anasema: Qur'ani Tukufu inalaani mara moja mantiki ya kishirikina na uigaji wa kipofu wa wahenga kwa kubainisha wazi kwamba baba zao hawakuelewa na pia hawakuongozwa. Yaani lau wazee wao wangeliongoka, ingekuwa sawa kufuata nyayo zao. Hata hivyo, wahenga wao hawakuwa na ufahamu wala hawakuwa na viongozi na waelekezi wanaojua. Itakuwa ni uharibifu kuiga wale ambao ni wajinga.

Katika Tafsiri yake ya Noor ya Qur'ani Tukufu, Hujjatul Islam Mohsen Qara'ati ameashiria baadhi ya mafunzo yanayoweza kupatikana kutokana na aya hii. Anasema Aya iliyotangulia imewatahadharisha wanadamu kuepuka kumfuata Shetani na Aya hii inataja mfano mmoja wapo wa njia ya Shetani ambayo ni kuigwa upofu.

Uigaji wa kimantiki na unaofaa hauzuiliwi. Kinachoharamishwa na Qur'ani Tukufu ni kuwaiga wale wasio na hekima wala hawakukubali uongofu wa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwongozo wa kimungu upo kila mahali na wakati.

Ujumbe wa Aya ya 170 ya Surah Al-Baqarah umebainishwa ifuatavyo katika Tafsiri ya Noor ya Qur'ani Tukufu

1- Irtija (kugeuka nyuma, au kupinga yaliyosahihi) ni marufuku. Kufuata njia na mapokeo ya wahenga na vizazi vilivyotangulia haikubaliki ikiwa hilo litafanyika bila ya kutafakari na kufikiri. (...Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu...)

2- Ubaguzi wa rangi na kabila ni miongoni mwa mambo yanayoweka msingi wa kutokubali ukweli.

3- Imani na mienendo ya wahenga au mababu huathiri maisha ya vizazi vijavyo.

4- Njia ya haki inaweza kupatikana kwa hikima na kwa Wahyi. (...baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka...).

5- Kupitisha uzoefu na maarifa kuna thamani, lakini kueneza ushirikina kutoka kizazi kimoja hadi kingine ni jambo lisilokubalika.

6- Akili inatuongoza kufuata Wahyi.

 

Habari zinazohusiana
captcha