IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /42

Sura Ash-Shura; Umuhimu wa Ushauri

19:12 - November 26, 2022
Habari ID: 3476149
TEHRAN (IQNA) – Zimetajwa sifa nyingi kwa waumini, na kila moja ya sifa hizo ina umuhimu wake. Mojawapo ya sifa za waumini ni kushauriana na wengine, jambo ambalo linaonekana kuwa na umuhimu maalum kwa sababu Sura moja ya Qur'ani Tukufu imepewa jina hilo.

Sura ya 42 ya Qur'ani Tukufu inaitwa Ash-Shura. Iko katika Juzuu ya 25 na ina Aya 53. Ash-Shura ni sura ya Makki na ni Sura ya 62 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno Shura (ushauri) lililotajwa katika aya ya 38 kama moja ya sifa za waumini: “Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho waruzuku wakawa wanatoa .”

Dhamira kuu ya Sura Ash-Shura ni suala la wahyi. Pia inazungumzia tauhidi, sifa nyingine za waumini na vilevile za makafiri na jinsi hali za kila kundi zitakavyokuwa Siku ya Kiyama.

Tawbah, Tauhidi, ufufuo, kumhimiza Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kubaki imara katika kuitangaza dini, kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu, umoja wa imani za Mwenyezi Mungu, kuzuia mifarakano baina ya watu, kusamehe makosa ya wengine, kuzuia hasira na kuhimiza  mashauriano katika masuala ya kijamii na kiserikali ni miongoni mwa mambo mengine ya sura hii.

Kwa ujumla, mada za Surah Ash-Shura zinaweza kugawanywa katika sehemu nne:

Sehemu ya kwanza, ambayo ndiyo kuu, inajadili ufunuo na uhusiano wa Mwenyezi Mungu na manabii. Sura inaanza na kumalizia na mada hii, na pia inashughulikia mada zinazohusiana kama vile utume wa Mtume Muhammad (SAW), Qur'ani Tukufu na mwanzo wa utume tangu zama za Nuhu (AS).

Sehemu ya pili inahusu masuala kama vile sababu za Tauhidi na ishara za Mwenyezi Mungu duniani.

Sehemu ya tatu inahusu ufufuo na hatima ya makafiri Siku ya Kiyama.

Mwisho, sehemu ya nne inahusu masuala ya kimaadili na kiakhlaqi huku ikihimiza Tawbah, msamaha, subira, uthabiti, na kuzuia hasira ya mtu, na kuonya dhidi ya majivuno, ukaidi, na kupenda sana mambo ya kidunia.

Habari zinazohusiana
captcha