IQNA

Waislamu India

Uuzaji wa mavazi ya Kiislamu umeongezeka ndia hata baada ya hujuma dhidi ya Hijabu

22:16 - December 01, 2022
Habari ID: 3476179
TEHRAN (IQNA) – Ripoti zinaonyesha kuongezeka kwa uuzaji wa nguo za Kiislamu nchini India huku kukiwa na marufuku ya hijabu ya Kiislamu kusini mwa nchi hiyo.

Katika njia iliyosongamana na shughuli nyingi ya vitongoji vya Delhi kusini, ni kanivali hapa kila siku. Watu humiminika kwenye soko hili kila jioni kununua kila kitu ambacho soko kuu linaweza kutoa.

Hapa ni kitovu cha ununuzi kati ya Waislamu wa mahali hapo.  Zaid muuza duka anasema soko hili ni maarufu sana, hasa miongoni mwa wanawake na katika mahitaji siku hizi ni mavazi ya Kiislamu ya miundo ya hivi karibuni.

Nguo kama vile abaya na hijabu, mavazi ya sala, buraq na naqaab, kanzu  na nguo za michezo zinauzwa kwa wingi.

Shagufta, mwanafunzi, anasema amechagua kuvaa Hijabu.  Anasema badala ya wanasiasa kujiingiza katika masuala ya Waislamu wakati wa kampeni za uchaguzi wanapaswa kusitisha  uhalifu wa chuki, na uteketezaji  nyumba za Waislamu. Wanaopinga Uislamu wanataka kuuonyesha ulimwengu kwamba Uislamu unahusu kuwakandamiza wanawake, lakini kwa hakika  Uislamu unawalinda wanawake, kuwalinda wanawake na kuwatendea kwa utu wa hali ya juu.

Kulingana na ripoti na tathmini za soko, soko la mavazi ya Kiislamu litaona ukuaji mkubwa ifikapo 2028. Mashirika mengi ya nguo yako katika mstari wa kutengeneza mavazi ya hivi punde ya Kiislamu yanayovuma.

Wanawake wengi wanaamini kwamba mzozo wa hijabu si chochote zaidi propaganda za kisiasa kabla ya uchaguzi ujao. Wanasema vyama vya siasa sasa vinatazamia kutumia masuala hayo ili kuwachochea watu wenye misimamo mikali kuwapigia kura.

Katika miezi ya hivi karibuni, marufuku ya hijabu ya Kiislamu kusini mwa India imekasirisha jamii ya Waislamu ambao wanasema ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya Uislamu katika hali ambayo katiba inalinda uhuru wa kidini.

Waangalizi wa mambo wanasema matamshi dhidi ya Uislamu yamepamba moto zaidi tangu chama tawala cha BJP kinyanyue mamlaka mwaka wa 2014.Chama hicho kina misimamo mikali ya Kihindu.

3481455

Kishikizo: india ، waislamu ، hijabu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha