IQNA

Ibada ya Umrah

Usajili wa alama za vidole kielektroniki kwa wanaotaka visa ya Umrah

17:48 - December 04, 2022
Habari ID: 3476195
TEHRAN (IQNA) – Usajili wa alama za vidole utakuwa wa lazima ili kutoa visa kwa wanaotaka kuingia Saudi Arabia kushiriki Hija ndogo ya Umrah.

Haya ni kwa mujibu wa Wizara ya Hija na Umrah ya Saudia iliyosema nchi hizo ni Uingereza, Tunisia, Kuwait, Bangladesh na Malaysia.

Uamuzi huo unalenga kurahisisha taratibu za kuingia kupitia bandari za Saudia na kuboresha matumizi ya kidijitali kwa Mahujaji.

Ili kusajili alama za vidole vyao, waombaji lazima kwanza wapakue programu ya ‘Saudi Visa Bio’ kwenye simu zao mahiri.

Kisha wanapaswa kuamua aina ya visa, kuingiza habari zao za pasipoti, kuchukua picha ya uso wao na kuifananisha na picha yao ya kibinafsi kwenye pasipoti, na kisha kuchambua alama za vidole vya vidole vyote 10 kupitia kamera.

3481513

Kishikizo: umrah saudia hija ndogo
captcha