IQNA

Waislamu Ujerumani

Matukio 120 ya uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu yaripotiwa Ujerumani Robo ya 3 ya 2022

23:05 - December 07, 2022
Habari ID: 3476213
TEHRAN (IQNA) – Visa 120 vya uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu viliripotiwa nchini Ujerumani katika robo ya tatu ya mwaka huu.

Uhalifu huo wa chuki ulisababisha watu kumi kujeruhiwa na misikiti kadhaa kuharibiwa.

Kulingana na jibu la serikali kwa swali la chama cha mrengo wa kushoto katika bunge la shirikisho la Ujerumani (Bundestag), ambalo lilichapishwa Alhamisi, idadi ya vitendo vya uhalifu katika robo ya kwanza vilikuwa 83 na 69 katika robo ya pili mtawalia.

Kwa mujibu wa serikali ya shirikisho, "hakuna mshukiwa" aliyekamatwa kuhusiana na mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu katika robo ya tatu. Mwendesha Mashtaka Mkuu katika Mahakama ya Juu ya Shirikisho pia "hajaanzisha mashtaka yoyote ya awali (...)."

Mashambulizi kumi na moja ya aina hiyo yalilenga misikiti. Kuumiza mwili, matusi, uchochezi wa chuki, uharibifu au matumizi ya alama zilizokatazwa zilikuwa aina nyingine za uhalifu dhidi ya Waislamu.

 Kuwa kawaida

Katika muongo mmoja hivi uliopita, ghasia dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani zimekuwa ukweli wa kawaida kwani kile kilichokuwa kikionekana kama watu wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia sasa wamepata uwakilishi wa kisiasa huku Wanazi mamboleo kadhaa wakishinda chaguzi na kuingia katika bunge la Ujerumani.

Kwa mfano, katika uchaguzi wa bunge wa 2013, chama cha Alternative for Germany (AfD) cha siasa kali za mrengo wa kulia kilikuwa kimepata zaidi ya kura 800,000 pekee na hakikuingia katika bunge la shirikisho la Ujerumani katika Bundestag.

Baada ya miaka minne, chama hicho kilipataa mafanikio makubwa - kupata zaidi ya kura milioni 5.3 huku kikiishia kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni.

Kwa vile kuwatukana walio wachache kuliwezeshwa na wanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia, kulisababisha kuongezeka kwa uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu.

3481568

captcha