IQNA

Jinai za Israel

Israel yaendeleza njama ya kufuta utambulisho wa Kiislamu wa Al-Quds

22:16 - December 08, 2022
Habari ID: 3476217
TEHRAN (IQNA) - Hivi karibuni utawala wa Kizayuni wa Israel uliondoa kuba na hilali ya mnara wa Ngome ya al-Quds (Jerusalem), kusini-magharibi mwa Mji Mkongwe.

Hatua hiyo ilizua hasira kubwa miongoni mwa Wapalestina, Kituo cha Habari cha Palestina kiliripoti.

Ngome ya al-Quds ni ngome ya kale iliyoko karibu na lango la Jaffa la Mji Mkongwe wa Quds. Muundo wa sasa ni ule wa usanifu majengo  wa zama za watawala wa zama za Ayyubi, Vita vya Msalaba, Mamluk, na Uthmaniya, pamoja na ngome ya kale ya Kirumi.

Kufuatia utawala haramu wa Israel wa kuikalia kwa mabavu al-Quds mwaka 1967, utawala huo ghasibu uliidhibiti ngome hiyo na kuigeuza kuwa jumba la makumbusho, baada ya kuipa jina la "Mnara wa Daudi" au "Makumbusho ya Historia ya Jerusalem". Utawala huo ulipiga marufuku Sala katika misikiti miwili ya Ngome hiyo iliyopo karibu na Lango la Hebron au Al Khalil (moja ya lango la Jiji la Kale).

Mkuu wa Kamisheni ya Kupambana na Uyahudishaji wa Quds, Nasser Al-Hadmi, alisema kuwa utawala haramu wa Israel unatumia visingizio vya ukarabati ili kuficha utambulisho wa Kiislamu wa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Aidha amesema msikiti huo wa kale ulijengwa na Sultan Al Nasir Muhammad bin Qawalunna kuongeza kuwa Israel haiwezi kubadlisha ukweli huo.

Halikadhalika amesema hatua  zaidi kazi za ‘ukarabati’ zinazotekelezwa na Israeli ni hujuma ya wazi kwenye eneo hili la kiakiolojia la Kiislamu.

Ili kuweka mambo wazi , mwaka 2016, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) lilipasisha azimio na kusema Mayahudi hawahusiki kivyovyote vile na maeneo matakatifu ya Quds ukiwemo Msikiti wa al Aqsa. Azimio hilo la UNIESCO lilisema wazi kuwa, maeneo hayo matakatifu ni ya Waislamu. Aidha Kamati ya Nnne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 202 ilipasisha azimio ambalo liliungwa mkono na nchi 139 na kutangaza kuwa, Msikiti wa Al Aqsa una utambulisho kamili wa Kiislamu na hauna uhusiano wowote na Mayahudi.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukipuuza nyaraka za kihistoria na maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu ukweli kuwa Msikiti wa Al Aqsa ni milki ya Waislamu. Upuuzaji huo ndio chanzo cha Israel kuendeleza sera zake za kutumia mabavu na ukatili dhidi ya Wapalestina ili kuwazuia kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa ambao pia unajulikana kama  Al-Haram Al-Sharif.

Ingawa uyahudishaji Msikiti wa Al Aqsa ni njama ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa miongo kadhaa sasa, lakini hatua ya Donald Trump, kutangaza mwaka 2017, alipokuwa rais wa Marekani,  kwamba anautambua mji wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, ilandaa uwanja kwa utawala wa Kizayuni kushadidisha utumiaji mabavu dhidi ya Palestina katika Msikiti wa Al Aqsa.

3481587

captcha