IQNA

Mgogoro katika utawala bandia

Muungano unaolegalega wa utawala wa Kizayuni wakaribia kusambaratika

22:12 - January 24, 2023
Habari ID: 3476459
TEHRAN (IQNA)-Duru za utawala wa Kizayuni wa Israel zimetangaza hbari ya kujiuzulu kiongozi mwingine wa serikali ya utawala huo bandia na hivyo kuongeza uwezekano wa kusambaratika muungano unaolegalega wa serikali yenye misimamo ya kufurutu ada ya Benjamin Netanyahu.

Kwa siku kadhaa sasa utawala wa Kizayuni unashuhudia mapambano baina ya serikali mpya yenye misimamo mikali na wapinzani. Jumamosi wiki hii kulifanyika maandamano makubwa ya zaidi ya watu laki moja ya kuipinga serikali hiyo.

Leo Jumanne, shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Moshe Hazan, mmoja wa wajumbe wa kamati ya fedha na akiba ya Benki Kuu ya Israel ambaye alikuwa mjumbe wa kamati hiyo ya watu sita tangu mwaka 2017 amejiuzulu akilalamika kuwa demokrasia iko hatarini na uchumi wa utawala wa Kizayuni unaelekea kusambaratika kabisa.

Vile vile amesema, kuna hatari serikali mpya ya Benjamin Netanyahu itazipoka uhuru wake taasisi za mahakama na huduma kwa jamii na hiyo ni hatari kubwa kwa demokrasia na uchumi wa Israel.

Wapinzani wa Netanyahu wanamshutumu nduli huyo wa mauaji ya Ghaza kwamba ana nia ya kuivunja nguvu idara ya mahakama ya utawala wa Kizayuni ili asalimike katika kesi ya ufisadi mkubwa inayomkabili yeye na mkewe.

Kabla ya hapo pia, mabalozi wa utawala wa Kizayuni katika nchi za Ufaransa na Canada walikuwa wameshajiuzulu kulialamikia serikali mpya ya Israel yenye misimamo ya kufurutu ada na walitangaza kumuunga mkono Yair Lapid, waziri mkuu wa zamani na kiongozi wa wapinzani wa Benjamin Netanyahu.

4116914

captcha