IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Pakistan yahimiza umoja wa kimataifa kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

18:24 - January 30, 2023
Habari ID: 3476490
TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Pakistan ametoa wito wa umoja wa kimataifa dhidi ya vitendo vya kudhalilisha matakatifu ya Kiislamu.

Shehbaz Sharif siku ya Jumapili alitoa wito kwa walimwengu waliostaarabika kulaani vikali vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu barani Ulaya.

Katika ujumbe wake wa Twitter, waziri mkuu alihimiza umoja wa kimataifa kupigana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia). "Kitendo cha mwanasiasa wa Denmark kuvunjia heshima Qur'ani ni tukio la tatu mfululizo ambalo linapaswa kulaaniwa vikali na ulimwengu uliostaarabika," Waziri Mkuu Sharif alitweet.

"Haja ya umoja wa kimataifa kupambana na chuki dhidi ya Uislamu haiwezi kuwa ya dharura kuliko ilivyo sasa," alisema na kuongeza, "Tumeumia sana."

Ofisi ya Mambo ya Nje ya Pakistan Jumamosi ililaani "kwa maneno makali" kitendo cha kudhalilisha Qur'ani Tukufu na mwanasiasa wa Denmark Rasmus Paludan siku moja kabla, kwa mujibu wa taarifa rasmi.

Ilisema "kurudiwa kwa kitendo hicho kiovu hakujaacha shaka katika fikra Waislamu kote ulimwenguni kwamba uhuru wa kujieleza unatumiwa vibaya ili kueneza chuki za kidini na uchochezi wa ghasia".

3482272

captcha