IQNA

Kwa mnasaba wa maadhimisha ya mwaka wa 44 wa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu azuru haram ya Imam Khomeini (MA) na maziara ya Mashahidi

18:37 - January 31, 2023
Habari ID: 3476493
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezuru haram toharifu ya Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kumuenzi na kumsomea Faatiha kiongozi huyo mwenye adhama kubwa wa taifa la Iran.
Sambamba na kuwadia maadhimisho ya AyyamuLlah ya Alfajiri Kumi na kutimia mwaka wa 44 wa ushindi adhimu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi alizuru haram tukufu ya mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo alimuenzi kiongozi huyo mwenye adhama kubwa wa taifa la Iran kwa kusali na kusoma Qur'ani kando ya haram yake.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alizuru pia maziara ya mashahidi  Beheshti, Rajai, Bahonar na mashahidi wa tukio la tarehe 7 Tir 1360, na kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aziinue zaidi daraja zao.
Katika ziara yake hiyo, Ayatullah Khamenei alizuru pia maziara ya Mashahidi wengine wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Miaka 44 iliyopita katika siku kama ya kesho ya tarehe 12 Bahman 1357 Hijria (tarehe 1 Februari 1979), Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alirejea nchini na kulakiwa kwa shauku kubwa na umati mkubwa wa watu na kukanyaga tena ardhi ya Iran ya Kiislamu baada ya kuwa mbali na nchi yake na kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka 15.

Siku kumi baada ya Imam Khomeini kuwasili Iran, yaani tarehe 22 Bahman 1357 (Februari 11, 1979), Mapinduzi matukufu ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi kamili.
Kwa sababu hiyo, kuanzia tarehe 12 Bahman, siku ambayo Imam Khomeini (MA) aliwasili nchini, hadi tarehe 22 Bahman, ambayo ni siku ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, imepewa jina la Alfajiri Kumi, ambapo kila mwaka hufanyika sherehe na hafla maalumu katika masiku hayo kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

4118514

captcha