IQNA

Taazia

Mitetemeko mikubwa ya ardhi yapelekea zaidi ya watu 2,500 kufariki Uturuki na Syria

20:25 - February 06, 2023
Habari ID: 3476519
TEHRAN(IQNA)- Watu wasiopungua 2,500 wamepoteza maisha kutokana na mitetemeko miwili mkubwa ya ardhi iliyoyakumba maeneo ya kusini mashariki mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria huku idadi ya wahanga wa janga hilo ikiongezeka kila sekunde kutokana na mamia ya watu kufunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Idadi rasmi ya vifo nchini Uturuki  hadi sasa ni  1,541. Hayo ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Kukabiliana na Maafa na Mambo ya Dharura nchini humo (AFAD) ambayo inatoa taarifa mpya takriban kila sekunde kuhusu idadi ya wahanga wa mitetemeko hiyo. Syria nayo imetangaza idadi rasmi ya waliopoteza maisha kuwa ni 810. Hatahivyo idadi isiyo rasmi katika nchi zote mbili ni 2,500 na huenda ikaongezeka huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

Serikali ya Uturuki imeambua kufunga skuli zote kote nchini humo hadi tarehe 13 Februari baada ya janga hilo.

Huko nchini Syria pia mamia ya watu wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na janga hilo lililokumbwa maeneo tofauti kama Ladhiqiyyah, Homs, na Halab. Taarifa za kina hazijapatikana hadi hivi sasa hasa kuhusu maafa yaliyotokea nchini Syria. 

Taarifa zinasema kuwa mtetemeko wa kwanza ulikuwa na ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rishta na umetokea saa kumi na dakika 17 alfajiri ya leo kwa saa za eneo hilo. Kitovu chake kilikuwa ni katika mji wa Gaziantep wa Uturuki ambapo mamia ya majengo yameporomoka.Masaa machache baadaye kulijiri mtetemeko mwingine wa ardhi uliokuwa na ukubwa 7.6 kwenye kipimo cha rishta.

Uturuki ni miongoni mwa nchi ambazo hukumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi mara kwa mara duniani. Mwaka 1999 watu 18,000 walipoteza maisha katika mtetemeko mkubwa wa ardhi kuwahi kuikumba nchi hiyo kwa miongo kadhaa.

3482366

Kishikizo: uturuki mtetemeko syria
captcha