IQNA

Tafsiri na Wafasiri wa Qur'ani Tukufu /16

Tafsiri inayojadili siri za kiroho za Qur’ani Tukufu

21:11 - February 06, 2023
Habari ID: 3476520
TEHRAN (IQNA) – Tafsiri ya Qur’ani Tukufu ya Gharaeb al-Qur’an na Ragheb al-Furqan ni tafsiri jumuishi ya Qu’rani Tukufu katika suala la kujadili siri za maneno na na siri za kiroho katika Qur’ani Tukufu.

Nizameddin Hassan ibn Muhammad Neyshaburi aliandika tafsiri hii kwa njia ya kimantiki na mbinu ya mwongozo inayoegemea kwenye mafundisho ya maneno na ya kiroho ya Qur’ani Tukufu.

Inaweza kuchukuliwa kama mojawapo ya tafsiri bora zaidi za Qur’ani ambazo zimeunda kiungo cha maana kati ya siri za maneno na siri za kiroho za Qur’ani Tukufu pamoja na dhahiri na batini yake.

Neyshaburi alikuwa nani?

Nizameddin Hassan ibn Muhammad Neyshaburi (aliyekufa takribani 1328 Miladia)  alijulikana kama Nizam A'araj. Yeye ni miongoni mwa wahifadhi mashuhuri wa Qur’ani Tukufu katika ulimwengu wa Kiislamu. Familia na kabila lake waliishi Qom lakini alizaliwa na kukulia Neyshabur (kaskazini mashariki mwa Iran). Wanachuoni walioishi baada yake wamebainisha fadhila, ujuzi, umahiri na utaalamu wake. Alikuwa mtaalamu wa sayansi ya kimantiki na katika lugha ya Kiarabu na fasihi.

Aliandika vitabu vingi kama Awqaf al-Quran na Lubb al-Ta’wil. Kazi yake kuu ni Gharaeb al-Quran na Ragheb al-Furqan.

Gharaeb al-Quran

Neyshaburi ametumia tafsiri ya Qur’ani ya Fakhr Razi na Kashhaf ya Zamakhshari katika kuandika tafsiri yake ya Qur’ani Tukufu.  Ametaja maoni yao na kuongeza  maoni yake mengi. Hadithi za Mtukufu Mtume (SAW) na riwaya kutoka kwa Maswahaba na Tabi’un zina nafasi maalum katika kitabu hiki.

Neyshaburi ameongeza pointi nyingi kwa zile zilizotajwa na Fakhr Razi na Zamakhshari, akikamilisha na wakati mwingine kukataa maoni yao. Kunapokuwa na tofauti ya maoni kati ya Fakhr Razi na Zamakhshari, Neyshaburi anatoa maoni yake juu ya nani kati yao anakubaliana naye.

Mwishoni mwa tafsiri yake ya Qur’ani, Neyshaburi anazungumza kuhusu kilichomsukuma kuandika tafsiri hiyo. Anasema aliiandika ili iwe swahiba wake katika maisha ya dunia hii na kesho akhera. Msukumo mwingine ulikuwa ni kukusanya maoni na mijadala yenye manufaa katika uwanja wa tafsiri ya Qur'ani, ikijumuisha yale kuhusu maneno na maana na kazi zake.

Juu ya kuchagua tafsiri ya Fakhr Razi kama mojawapo ya vyanzo vyake, anaandika kwamba kazi ya Fakhr Razi inajumuisha mijadala yenye manufaa lakini pia ina nukta ambazo ni ngumu kufahamu. Ndio maana Neyshaburi aliamua kuachana na yaliyomo ngumu na ambayo sio muhimu sana na kutoa iliyobaki kwa wasomaji katika muundo mfupi na wazi.

Mbinu ya Tafsiri

Katika tafsiri hii ya Qur’ani, Neyshaburi ana mbinu yake mwenyewe. Mwanzoni mwa kila Sura, anatoa maelezo ya jumla kuhusu jina la sura, kuwa ni Makki au Madani, na idadi ya aya, maneno na herufi. Kisha anataja usomaji tofauti kuhusu kila aya.

Moja ya sifa za kazi hii ni uainishaji wake wa yaliyomo kwa njia tofauti katika mada mbalimbali na kila mada katika masuala kadhaa.

Mwandishi wa Rawzat al-Jannat anasema tafsiri ya Qur’ani ya Neyshaburi kama mojawapo ya tafsiri bora zaidi za Qur’ani ambacho kinajumuisha nukta za kiroho na faida za dhahiri na batini.

captcha