IQNA

Arbaeen ya Imam Hussein AS

Washindi wa Tuzo ya Nane ya Kimataifa ya Arbaeen Watajwa

22:04 - February 06, 2023
Habari ID: 3476523
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa toleo la 8 la Tuzo la Kimataifa la Arbaeen walitangazwa na kutunukiwa katika sherehe hapa Tehran siku ya Jumatatu.

Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) iliandaa hafla hiyo iliyohudhuriwa na maafisa kadhaa kama vile Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Mohammad Mehdi Esmaeili na Mkuu wa ICRO Hojat-ol-Islam Mohammad Mehdi Imanipour, pamoja na wageni kutoka Iran na  nchi nyingine.

Washiriki kutoka nchi 20 walikuwa wamewasilisha kazi kuhusu Arbaeen katika nyanja kama vile upigaji picha, video, na safari, vitabu na mitandao ya kijamii.

Katika upigaji picha, Mohammad Ibrahim Abdel Amir kutoka Iraq na Hamid Abedi kutoka Iran walitangulia.

Katika sehemu ya vitabu, Hadi Ghiyasi na Mohammad Nasravi kutoka Iran kwa pamoja walishinda tuzo ya juu.

Batul Zahra Akyul kutoka Uturuki alinyakua tuzo ya juu zaidi katika uwanja wa kumbukumbu za safari huku Sajjad Mahmoudi kutoka Australia na Seyed Nematollah Esmaeili kutoka Iran wakiibuka wa kwanza katika kategoria ya video.

ICRO imeandaa Tuzo la Arabeen tangu 2014 kwa lengo la kuakisi maonyesho ya tukio hili la kidini la kimataifa kwa ulimwengu.

Popote ambapo maneno hayawezi kuwasilisha ukuu wa ujumbe, njia bora ya mawasiliano itakuwa lugha ya sanaa. Ndio maana ICRO iliamua kushikilia tuzo hiyo ya kimataifa kila mwaka katika kategoria za picha, video, na orodha za safari, kwa lengo la kueneza ujumbe wa Arbaeen na Ashura.

Arbaeen, ambayo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani, inakuja siku 40 baada ya Ashura, kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam wa tatu wa Mashia na Mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS.

Kila mwaka umati mkubwa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na pia wasiokuwa Mashua humiminika katika mji wa Karbala nchini Iraq, ambako ndiko kunako kabur takatifu la Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo huko Arbaeen.

Wafanyaziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri njia ndefu kwa miguu hadi Karbala

Mnamo Septemba 2022, idadi kubwa ya watu kutoka nchi tofauti walishiriki katika mila ya Arbaeen, na kuweka rekodi mpya.

 

4120084

captcha