Hapa chini tunamsikiza qarii maarufu wa Misri Sheikh Abdul Basit Abdul Samad akisoma aya ya 21 ya Sura Az-Zumar na ni moja ya aya ambamo Mungu anaangazia jinsi maji yatokayo angani yanavyobadilisha uso wa dunia.
"Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchem katika ardhi, kisha kwa maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano, na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili. "