IQNA

Harakati za Qur'ani Misri

Wito wa kupiga marufuku matangazo ya biashara katika  Idhaa ya Qur'ani ya Misri

14:15 - March 23, 2023
Habari ID: 3476748
TEHRAN (IQNA) - Wanaharakati, wanasiasa na wasikilizaji nchini Misri wametoa wito wa kupigwa marufuku matangazo ya biashara kwenye Idhaa au Redio ya Qur'ani ya nchi hiyo.

Wanasema matangazo hayo yanaharibu hali ya kiroho ambayo inapaswa kutawala vipindi vya kituo hicho cha redio, imeripoti Al Jazeera.

Ulfat al-Mizlawi, mbunge, ni miongoni mwa wanaotaka kupigwa marufuku matangazo ya biashara, akisema hali ya Qur'ani ya vipindi vya redio hiyo haipaswi kuhujumiwa na matangazo ya biashara.

Kile ambacho watu hutazama na kusikiliza kwenye vituo vingine vya TV na redio ni tofauti na kile wanachosikiliza kwenye Redio ya Quran, Mizlawi alisema.

Ammar Ali Hassan, mwandishi, alisema dhamira ya Redio ya Qur'an ni kukata kiu ya kiroho ya wasikilizaji na utangazaji wa matangazo ya biashara kwenye redio hauendani na lengo hili.

Pia, Yahya Sayyed an-Najjar, mtumiaji wa Twitter, aliandika kwenye tweet kwamba kuendesha matangazo ya biashara kwenye redio ya Qur'ani ni sawa na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.

Redio ya Qur’ani ni idhaa maarufu nchini humo Misri, huku Wamisri wengi wakisikiliza visomo, hotuba na vipindi vya tafsiri ya Qur'ani vinavyotangazwa humo.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Kituo cha Mafunzo ya Vyombo vya Habari na Maoni ya Umma cha nchi ya Kiarabu mwishoni mwa 2020, ni kituo cha pili cha redio maarufu nchini Misri.

Utangazaji wa matangazo kwenye redio ulianza mwaka wa 2014. Katika mwaka huo, Umoja wa Vituo vya Redio na TV ulisema umepokea maombi mengi kutoka kwa makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuendesha matangazo kwenye Redio ya Qur'ani, ambayo ina idadi kubwa ya wasikilizaji.

3482906

Kishikizo: misri idhaa ya qurani
captcha