IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Qarii wa Qur'ani ni mfikishaji wa ujumbe na risala ya Mwenyezi Mungu, ana haja ya kuwa na sauti nzuri

6:09 - March 24, 2023
Habari ID: 3476750
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Qarii wa Qur'ani ni mfikishaji wa ujumbe na risala ya Mwenyezi Mungu na ili kufikisha ujumbe huo kwa njia nzuri ana haja ya kuwa na sauti nzuri na usomaji bora kabisa.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo Alhamisi mjini Tehran wakati alipohutubia mahafali ya qiraa ya Qur'ani katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kubainisha umuhimu mkubwa wa kusoma na kutafakari juu ya aya za kitabu kitukufu cha Qur'ani.

Kiongozi Muadhamu amekumbusha kwamba, watu wanapaswa kuzingatia kwamba, kusoma Qur'ani si jambo la kiburudisho bali ni hatua na amali inayoongeza imani.

Kuhusiana na umuhimu wa kusoma Qur'ani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwamba, 

Waislamu wanapaswa kusoma Qur'ani kila siku hata kama ni kwa kiwango kidogo, na haimpasi Mwislamu impite siku katika mwaka ambayo hajasoma Qur'ani tukufu.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, usomaji Qur'ani unapaswa kuandamana na utakafari na kufahamu maana ya maneno haya ya Mwenyezi Mungu.

Kiongozi Muadhamu amewaasa wasomaji na maqarii wa Qur'ani kwa kuwaambia, usomaji Qur'ani unapaswa kuwa kwa namna ambayo utakuwa na taathhira kwa anayesomewa na hii ina mbinu na ubunifu.

Aidha, Ayatullah Khamenei, ameitaja Qur'ani kuwa ni kitabu cha maisha, itabu cha hekima, muongozo na kwamba, kila ukurasa wa Qur'ani ni darsa na funzo kwa maisha binafsi, ya kijamii na kadhalika na yote haya ni hekima na hivyo Waislamu wananapaswa kutumia vyema fursa ya kuwa na kitabu hiki.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu halikadhalika amesema kuwa, hii leo idadi ya wasomaji mahiri wa Qur'ani tukufu imeongezeka sana katika Jamhhuri ya Kiislamu ya Iran ikilinganishwa na kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

4129616

Habari zinazohusiana
captcha